Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Michezo ya marudiano hatua ya 16 bira ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imeendelea tena usiku wa March 9, kwa michezo miwili kupigwa barani Ulaya. Klabu ya Chelsea ilikuwa mwenyeji wa klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa, wakati Zenit walicheza dhidi ya Benfica.
Kwa upande wa klabu ya Chelsea walikuwaStamford Bridge chu kupambana na PSG ili waweze kusonga mbele hatua robo fainali kwa kuhangaika kutaka kuifunga klabu hiyo, ambayo mchezo wa kwanza, walifungwa 2-1Paris Ufaransa.

Hata hivyo jitihada za Chelsea ziligonga mwamba, baada ya PSG kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1, hivyo Chelsea wametolewa kwa jumla ya magoli 4-2. Magoli ya PSGyalifungwa na Adrien Rabiot dakika ya 16 naZlatan Ibrahimovic dakika ya 67 na Chelseakuambulia goli moja pekee lililofungwa naDiego Costa dakika ya 27.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment