TAMISEMI yakanusha uvumi kuhusu ajira mpya za walimu | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Friday, March 11, 2016

TAMISEMI yakanusha uvumi kuhusu ajira mpya za walimu

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

TAARIFA KWA UMMA
Kumekuwa na taarifa za upotoshaji zinasombazwa kwenye mitandao ya kijamii juu ya kutolewa kwa ajira mpya ya walimu kwa shule za sekondari na msingi kwa mwaka 2015/2016.

Taarifa hizo zinazosambazwa zinaeleza kwamba walimu wapatao 17,928 wa cheti (Daraja IIIA) , 5,416 wa Stashahada kwa sekondari na 12,677  kwa  shule za mazoezi za vyuo vya ualimu Tanzania Bara wamepangwa kwa ajili ya kuanza kazi.

Katika taarifa hiyo inawataka walimu hao waliopangwa kuripoti kwa Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kupangiwa vituo vya kazi na kuanza kazi tarehe 01/04/2016.

Taarifa hizo pia zinaeleza kuwa walimu ambao hawataripoti ifikapo tarehe 10/04/2016 hawatapokelewa tena na watakuwa wamepoteza ajira zao.

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inapenda kuchukua nafasi hii kukanusha taarifa hizo kuwa ni za upotoshaji. Wananchi wanapaswa kuzipuuzia kwani mpaka sasa bado Serikali haijatoa ajira za walimu kwa mwaka 2015/2016.

Ajira mpya za ualimu zitakapokuwa tayari zitatangazwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari na katika tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ambayo ni www.tamisemi.go.tz.
 

Imetolewa na :
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
11/03/2016
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA