Tanzania yalaani kitendo cha meno ya Tembo yaliyochomwa moto nchini Malawi | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Wednesday, March 16, 2016

Tanzania yalaani kitendo cha meno ya Tembo yaliyochomwa moto nchini Malawi

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Serikali imeanza mazungumzo na Ubalozi wa Malawi nchini baada ya nchi hiyo kuteketeza tani 2.6 za meno ya tembo yaliyotoka Tanzania.
Serikali inafanya mazungumzo hayo ili kuzuia kuchomwa kwa meno mengine yaliyopo nchini humo kwa kuwa ni kielelezo kinachohitajika mahakamani.
Mkurugenzi wa Wanyamapori wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Herman Keraryo alisema mwanasheria wa wizara alifanya mawasiliano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ubalozi huo ili kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Malawi.
Idadi ya vipande vya meno ya tembo vilivyokamatwa nchini  Malawi ni 781 na thamani yake inakisiwa kuwa  bilioni 3.
Katika hatua nyingine; Serikali ya Kenya inatarajia kuteketeza tani 120 za meno ya tembo mwishoni mwa mwezi huu baada ya kuyakamata nchini humo.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA