UN: Saudia inawalenga raia katika vita nchini Yemen | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Saturday, March 19, 2016

UN: Saudia inawalenga raia katika vita nchini Yemen

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
UN: Saudia inawalenga raia katika vita  nchini Yemen
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa amesema Saudia na waitifaki wake wanadondosha mabomu katika shule, mahospitali na vituo vya afya nchini Yemen.
Zeid Raad al-Hussein, Kamishna wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa katika ripoti yake siku ya Ijumaa ameongeza kuwa: "Katika hujuma za muungano wa kijeshi wa Saudia dhidi ya Yemen tokea Machi 2015, katika hujuma kwa maeneo yasiyo ya kijeshi raia wapatao 3,218 wameuawa. Aidha amesema watu wengine 5,778 wamejeruhiwa katika hujuma hizo. Maafisa wa Yemen wanasema watu 8,500 wameuawa katika hujuma za mwaka moja wa Saudia dhidi ya nchi hiyo.
Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa ameaalni vikali hatua ya hivi karibuni ya jeshi la Saudia kuhujumu soko moja katika mkoa wa Hajja nchini Yemen ambapo watu 106 waliuawa wakiwemo watoto 24.
Jana makumi ya maelfu ya wananchi wa Yemen waliandamana  katika mji mkuu wa nchi hiyo Sana'a kulaani siasa za kichokozi na kivamizi za utawala wa Aal Saud.
Katika maandamano hayo wananchi wa Yemen mbali na kulaani utawala wa Aal Saud na Marekani wamelaani mashambulio ya anga yaliyofanywa dhidi ya soko mkoani Hajja.
Tangu mwezi Machi mwaka 2015 hadi sasa Saudi Arabia imeiwekea mzingiro wa angani na baharini Yemen na kuzuia misaada ya kibinadamu isiwafikie wananchi wa nchi hiyo, lengo likiwa ni kuindoa madarakani harakati ya wananchi ya Ansarullah na kumrejesha madarakani kibaraka wake Abd Rabbuh Mansour Hadi.
Mashambulio ya Saudia dhidi ya Yemen yameangamiza na kusababisha hasara kubwa pia kwa miundombinu ya Yemen, mbali na kulenga na kubomoa hospitali, shule, nyumba za raia na misikiti nchini humo.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA