Utalii wa ndani kitendawili Tanzania | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Friday, March 11, 2016

Utalii wa ndani kitendawili Tanzania

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Kufuatia suala la utalii wa ndani kuendelea kuzorota katika nchi nyingi za Afrika,baadhi ya asasi binafsi na makampuni ya utalii Tanzania,yameanza kutafuta mikakati ambayo itasaidia kuamsha ari ya raia kutembelea vivutio vyao na kuachana na dhana kudhani kuwa utalii ni kwaajili ya wanaotoka nchi za Ulaya tu.
Nchini Tanzania kampuni ya Utalii ya Kili Base Adventures imezindua Tamasha maalumu linalotarajiwa kufanyika kila mwaka ambapo katika tamasha hili mwana ndondi wa mstaafu wa ngumi za kulipwa Rashid Matumula anatarajiwa kuongoza hamasa hiyo ambayo itahitimishwa na watalii wazawa kuupanda mlima Kilimanjaro.
Sifael Malle ni mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya Kili Base Adventures,ambaye amesema kuwa kutokana na utafiti wao wamebaini kuwa raia wengi katika nchi za Afrika Mashariki hawaoni umhimu wa kufanya utalii wa ndani japo kuwa hawana ueledi mkubwa wa vivutio vilivyo katika maeneo yao.
“Unajua mfano kama Tanzania mtu unakuta kuzaliwa hadi kufikia uzee wake hajawahi fika kwenye vivutio,lakini mbaya zaidi ni pale wanapokuwa nje ya nchi zao unakuta mtu anaulizwa kivutio kilicho katika nchi yake haelewi wakati watu wanatoka katika mabara ya mbali wanafahamu mfano mlima Kilimanjaro ama hifadhi ya taifa”amesema Malle.
Akizungumzia serikali za Afrika na Afrika Mashariki katika mikakati ya kuhamasisha utalii wa ndani,mkurugenzi huyo wa kampuni ya Kili Base Adventure anasema zinapaswa kuwana mikakati zaidi ili kuweza kuamsha ari ya wananchi wake kuona umhimu wa kufanya utalii wa ndani.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA