Wakuu wa Idara wapewa masaa 24 kupeleka ripoti ya matatizo ya wananchi | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Wednesday, March 16, 2016

Wakuu wa Idara wapewa masaa 24 kupeleka ripoti ya matatizo ya wananchi

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewagiza wakuu wa idara wa Halmashauri za jiji la Dar es Salaam kutoa ripoti za matatizo ya wananchi na jinsi walivyojipanga ndani ya masaa 24.
Makonda ameyasema hayo wakati akizungumza na watendaji wa halmashauri hizo ikiwa ni siku ya kwanza kuingia katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa baada ya kuapishwa jana.
Makonda amesema wananchi wa Dar es Salaam wanakabiliwa na changamoto za ulinzi,maji,biashara pamoja na elimu  hivyo lazima matatizo hayo yapate ufumbuzi katika kusaidia wananchi kuondokana na changamoto hizo.
Makonda amesema kuwa kwa muda alioutoa wa masaa 24 ni mkubwa hivyo lazima wafanye kazi hiyo jinsi walivyojipanga katika kutatua changamoto hizo.
Amesema wakati umefika katika kuwatumikia wananchi kuwaondolea  kero zao ambazo zinafanya kuwa na malalamiko yasioisha.
Makonda amesema amekutana na Kamanda wa Polis wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro kuzungumzanaye juu ya suala la ulinzi na usalama  kwa wananchi.
Aidha amesema kuwa kukutana huko sio mara ya kwanza ataendelea ikiwa ni lengo la kuwatumikia wananchi pamoja na kutatua kero zao.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA