Waliokufa baada ya kuporomoka jengo Nigeria ni 30 | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Thursday, March 10, 2016

Waliokufa baada ya kuporomoka jengo Nigeria ni 30

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Waliokufa baada ya kuporomoka jengo Nigeria ni 30
Idadi ya waliopoteza maisha baada ya jengo lenye ghorofa 5 kuporomoka katika mji mkuu wa kibiashara wa Nigeria, Lagos imepindukia 30.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nigeria imesema kuwa, jengo hilo ambalo lilikuwa linaendelea kujengwa liliporomoka Jumanne iliyopita, kutokana na ukiukaji wa kanuni za ujenzi. Imesema kuwa, jengo hilo liliporomoka baada ya mmiliki wake kuamua kuongeza ghorofa za ziada pasina idhini ya mamlaka husika. Awali iliripotiwa kuwa watu 4 tu ndio waliokuwa wameaga dunia katika mkasa huo lakini kufikia jana jioni baada ya shughuli za kupekua vifusi kukamilika, miili zaidi ilipatikana.
Aidha watu 13 walipatikana wakiwa hai katika shughuli hizo jana Jumatano. Taarifa hiyo ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nigeria imemtaka mmiliki wa jengo hilo kupiga ripoti mara moja katika kituo chochote cha polisi la sivyo mkono wa sheria utafuata mkondo wake.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA