Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Wanajeshi wa Urusi wameanza kuondoka Syria siku moja baada ya Rais Vladimir Putin kushangaza wengi kwa kutangaza kwamba wanajeshi wa nchi yake wangeondoka nchini humo.
Kundi la kwanza la ndege za kivita za nchi hiyo limeondoka kutoka kambi ya Hmeimim nchini Syria mapema asubuhi, wizara ya ulinzi ya Urusi imesema.
Mataifa ya Magharibi yamefurahia hatua hiyo, ingawa kwa tahadhari, yakisema itaishinikiza serikali ya Syria kushiriki kwenye mazungumzo.
Mazungumzo ya amani yanayolenga kumaliza mzozo nchini humo yameingia siku yake ya pili leo.
Hayo yakijiri, tume ya Umoja wa Mataifa inatarajiwa kutoa ripoti ya kutekelezwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita nchini Syria baadaye leo.
Hatua ya kuondolewa kwa baadhi ya wanajeshi wa Urusi nchini Syria ilitangazwa Jumatatu wakati wa mkutano kati ya Bw Putin na mawaziri wake wa ulinzi na mashauri ya kigeni.
Bw Putin alisema majeshi hayo yametimiza lengo lililokusudiwa.
Urusi ni mshirika mkubwa wa Rais wa Syria Bashar al-Assad, na afisi yake imejaribu kuondoa uvumi kwamba kumezuka tofauti baina ya nchi hizo mbili, na kusema uamuzi huo ulifikiwa kwa pamoja.
Operesheni ya kijeshi ya Urusi ilianza Septemba mwaka jana na kuisaidia sana serikali ya Syria ambayo ilifanikiwa kukomboa maeneo kutoka kwa waasi.
Kwa mujibu wa waziri wa ulinzi Sergei Shoigu, kama alivyonukuliwa na vyombo vya habari vya Urusi, ndege za kivita za taifa hilo lilifanya safari 9,000 na kusaidia kukombolewa kwa maeneo 400 ya makazi.
Jeshi la Urusi, amesema Bw Shoigu, lilisaidia serikali ya Bw Assad kukomboa eneo la kilomita mraba 10,000.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment