Boko Haram 300 wauawa, raia 2000 wakombolewa | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Wednesday, April 6, 2016

Boko Haram 300 wauawa, raia 2000 wakombolewa

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

 Muungano wa kijeshi unaopambana na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Boko Haram umetangaza kuwa, wapiganaji 300 wa kundi hilo wameangamizwa na karibu raia 2000 wasio na hatia wamekombolewa kutoka mikononi mwa magaidi hao.  Muungano huo umetangaza kuwa wapiganaji hao 300 wa kundi la kigaidi la Boko Haram wameuawa katika operesheni ya kijeshi iliyofanyika karibu na mpaka wa Nigeria na nchi za Cameroon na Chad. 
Kamanda Mcanerooni wa operesheni hiyo, Bouba Dobekreo, amesema kuwa operesheni hiyo imelenga na kuharibu kabisa kambi ya Boko Haram iliyokuwa ikitumiwa kutengeza mabomu iliyopo yapata kilomita 35 kutoka kwenye mji wa Kumshe na kwamba magari na zana za kijeshi za kundi hilo zimechukuliwa ngawira.  Askari 9000 wanashiriki katika muungano dhidi ya Boko Haram unaoshirikisha nchi za Cameroon, Nigeria, Chad, Niger na Benin.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA