LEO NI KARUME DAY: KUMBUKUMBU YA MIAKA 44 ya KIFO CHA SHEIKH AMANI ABEID KARUME | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Thursday, April 7, 2016

LEO NI KARUME DAY: KUMBUKUMBU YA MIAKA 44 ya KIFO CHA SHEIKH AMANI ABEID KARUME

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Leo April 7, 2016 ni siku ya kumbukumbu ya miaka 44 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ambaye alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi. 
Mzee Karume aliongoza nchi baada ya mapinduzi yaliyomwangusha Sultani aliyekuwa akitawala Zanzibar hadi mwanzoni mwa mwaka 1964. 
Baada ya miezi mitatu Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Nyerere. Baada ya Muungano wa nchi hizi mbili uliozaa Tanzania, Mzee Karume alikuwa Makamu wa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.






 Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati 
                                           Sheikh Abeid Amani Karume
 Hapa ndipo alipouwawa Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume miaka 44 iliyopita ndani ya ofisi za Makao Makuu ya CCM Kisiwandui, Unguja, wakati akicheza bao na marafiki zake. Matundu yanayoonekana ukutani ni ya risasi ambayo muuaji alimimina kabla na yeye kuuwawa kwa kupigwa risasi na walinzi wa Hayati Karume. Sehemu hii imewekwa uzio maalumu ili kupahifadhi kama kumbukumbu, kwani kila kitu kipo vile vile kilivyokuwa siku hiyo
Wanafunzi wakitembelea mahali alipouwawa Hayati Mzee Karume.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA