Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Mtangazaji Mahiri katika Vituo kadhaa vya Radio hapa nchini, Gardner G. Habash ametangaza rasmi kurejea katika Kituo chake cha kazi cha awali,CloudsFM na kuendelea kuunguruma katika kipindi chake kile kile cha JAHAZI kama ambavyo anavyosikika akitangaza hivi sasa ndani ya kipindi hicho.
Gadna anaendelea kuunguruma akiwa sambamba na swahiba wake, Ephrahim Kibonde pamoja na wengine. Pichani juu ni mtangazaji huyo Gardner G Habashi akimwaga wino kuashiria sasa jahazi liko tayari kuanza kukata mawimbi ya bahari,kulia kwake ni Mkuu wa Vipindi wa sasa wa Radio hiyo, Shafih Dauda.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
Post a Comment