Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(katikati), akiongozana na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma, SACP Sabas Matolo(kushoto) na Mkuu wa Gereza la Bangwe,SSP Raphael Mwanyingile(kulia), alipofika kutembelea gereza hilo katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma tarehe 31/3/2016.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akisaini kitabu cha wageni katika Gereza la Bangwe mkoani Kigoma, ambapo baadae alisikiliza risala iliyohusu mambo mbalimbali, iliyoandaliwa na wafungwa na mahabusu walioko katika gereza hilo na kuahidi kushughulika changamoto zao.
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma, SACP Sabas Matolo, akisoma taarifa ya hali ya magereza mkoani Kigoma mbele ya Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni.Naibu Waziri yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.
Mmoja wa Askari Magereza mkoa wa Kigoma, akizungumza wakati wa kipindi cha maswali kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani).Naibu Waziri alifanya mkutano na watumishi wa Idara zote zilizopo chini ya Wizara, mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Hifadhi ya Jamii(NSSF),mkoani Kigoma.
Watumishi wa Idara zilizopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii(NSSF), mjini Kigoma.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment