Waasi wadungua ndege ya jeshi la Syria | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Wednesday, April 6, 2016

Waasi wadungua ndege ya jeshi la Syria

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

ImageWaasi wadungua ndege ya jeshi la Syria

Makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Syria yamepata pigo kubwa baada ya waasi ambao ni washirika wa wanamgambo wa al-Qaeda nchini Syria kudungua ndege ya jeshi la Syria iliyokuwa ikipeleleza maficho ya waasi karibu na mji wa Aleppo.
Yamkini wanamgambo wa al Nusra Front wamechapisha video mtandaoni inayoonesha rubani wa ndege ya kijeshi Syria aliyetekwa nyara baada ya kudunguliwa kwa ndege yake.
Hili ni tukio la pili baada ya ndege nyingine ya kijeshi kudunguliwa mwezi Machi.
Waasi hao wanaoungwa mkono na Marekani wamekuwa wakiomba msaada wa makombora yenye uwezo wa kudungua ndege ilikujikinga dhidi ya mashambulizi ya angani yanayotekelezwa na jeshi la Syria na washirika wake wakiongozwa na Urusi.

ImageAFP
Imageal Nusra Front wamechapisha video mtandaoni inayoonesha rubani wa ndege ya kijeshi Syria aliyetekwa

Katika video hiyo rubani huyo anaonekana akitaja jina lake na sehemu anayotokea ambayo ni Latakia
Jeshi la Bashar al Assad limekiri kupoteza ndege hiyo na pia rubani wake aliyekwepa kwa mwavuli lakini kwa bahati mbaya akatekwa nyara.
Shirika la kupigania haki za kibinadamu Syrian Observatory for Human Rights limesema kuwa rubani huyo amefungiwa katika makao makuu ya Al Nusra Front.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA