Jose Mourinho to Man United – Done Deal | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Sunday, May 22, 2016

Jose Mourinho to Man United – Done Deal

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Hatimaye tetesi zinageuka kuwa kweli, Manchester United watamtangaza Jose Mourinho kuwa kocha wao, shirika la utangazaji la Uingereza BBC limeripoti.
  Mourinho amekuwa nje ya kazi tangu alipofukuzwa kazi na Chelsea mnamo December 2015. 
Huku United wakiwa wameshindwa kufuzu kucheza Champions League chini ya Louis van Gaal – viongozi wa Old Trafford wameamua kufanya mabadiliko. 
Inaeleweka dili na kocha huyo mwenye miaka 53 lilifanyika kabla ya mchezo wa fainali ya FA Cup dhidi ya Crystal Palace.
United wanategemewa kumtangaza rasmi Mourinho mapema wiki ijayo baada ya kumtaarifu Van Gaal kuhusu mwisho wa ajira yake. 
Van Gaal bado ana mwaka mmoja kwenye mkataba wake wa miaka 3, lakini pamoja na kutumia £250m utawala wake umekuwa wa majuto kwa klabu na kuwaacha mashabiki wengi wakiwa hawaridhiki na utendaji wake, msimu wa kwanza alimaliza nafasi ya 4, na msimu huu watano.  
 
Mourinho ni mmoja wa makocha bora katika ulimwengu wa soka, akishinda makombe matatu ya ligi katika vipindi viwili vya kazi ndani ya Chelsea, pamoja kuziongoza Porto na Inter Milan kutwaa Champions League – pia akibeba ubingwa wa La Liga na RealMadrid. 
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA