Majina Ya Kidato Cha Sita 2016 Wanaotakiwa Kujiunga Na JKT Kwa Mujibu Wa Sheria......Tarehe ya Kuripoti Kambini ni Tarehe 1 Hadi 5 Juni | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Sunday, May 22, 2016

Majina Ya Kidato Cha Sita 2016 Wanaotakiwa Kujiunga Na JKT Kwa Mujibu Wa Sheria......Tarehe ya Kuripoti Kambini ni Tarehe 1 Hadi 5 Juni

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2016, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria. 


Sanjari na uchaguzi huo, JKT limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01 - 05 Juni 2016. 


Vijana waliochaguliwa, wamepangiwa katika Kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT Makutupora – Dodoma, JKT Mafinga – Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila – Kigoma. 


Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) wanatakiwa kuripoti Kambi ya JKT RUVU, iliyopo Mlandizi mkoani Pwani, ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo. 


JKT linawataka vijana hao kuripoti makambini wakiwa na nguo za michezo kama vile ‘track suit’, bukta, raba pamoja na nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa kwenye makambi yenye baridi kama JKT Makutupora, JKT Mafinga, JKT Mlale, JKT Kanembwa na JKT Mtabila. 


Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote waliochanguliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, uhodari, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu. 


Imetolewa na: 
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano 
Makao Makuu ya JKT 


Tarehe 20 Mei 2016

HAYA HAPA BOFYA KWENYE LINKS HIZO CHINI

Majina Ya Wanafunzi 1400 Kidato Cha 6 Waliochaguliwa JKT Kambi ya Msange -Tabora

 

Haya Hapa Majina Ya Wanafunzi 1700 Kidato Cha 6 Waliochaguliwa JKT Kambi ya Bulombora-Kigoma

 

Haya Hapa Majina Ya Wanafunzi 1500 Kidato Cha 6 Waliochaguliwa JKT Kambi ya Rwamkoma - Mara

 

Haya Hapa Majina Ya Wanafunzi 1500 Kidato Cha 6 Waliochaguliwa JKT Kambi ya Kanembwa- Kigoma

 

 

KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA