Mpinzani wa Donald Trump, John Kasich ajiondoa | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Thursday, May 5, 2016

Mpinzani wa Donald Trump, John Kasich ajiondoa

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Mpinzani mkuu wa Donald Trump katika kinyang'anyiro cha tikiti ya urais wa chama cha Republican , John Kasich amejiondoa mashindanoni.

Gavana huyo wa jimbo la Ohio ametangaza kusitisha kampeini zake baada ya kura ya maoni kuonesha kuwa umaarufu wake hauwezi kumpiku bwenyenye huyo mbishi anayepigiwa upatu kutwaa tikiti ya chama cha Republican kuwania urais wa Marekani.

Licha ya kushindwa kupata uungwaji mkono mkubwa wa wajumbe wa chama cha Republican, Gavana Kasich ameahidi kuwaomba rasmi wajumbe katika kongamano la kitaifa la chama hicho mwezi Julai, Bw Trump anapigiwa upatu kutawazwa mgombea wa Republican.

Kwa upande wake Kasich hakushinda jimbo lolote isipokuwa lake la Ohio.
Mpinzani mweza ambaye ni Seneta wa jimbo la Texas Ted Cruz naye alijiondoa mapema wiki hii kufuatia kushindwa kwake na bw trump katika jimbo la Indiana.

Gavana Kasich amefutilia mbali mikutano ya hadhara ya kampeini katika jimbo ya Washington. Mapema leo bw Kasich alizindua nembo yake iliyoundwa kwa mfano wa filamu maarufu ya Star-Wars ambapo alijieleza kuwa ndiye aliyesalia pekee yake dhidi ya Donald Trump.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA