Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi, alithibitisha kuwashikilia watu hao na alisema majina yao yanahifadhiwa kwa kuwa wanamtafuta Shaffy Rashid kwa tuhuma za kumtorosha mwanafunzi huyo.
Ollomi alisema kuwa Aprili 21 mwaka huu, mwanafunzi huyo alitoroka nyumbani kwao eneo la Nshambya na kuelekea kusikojulikana na kuwa baadaye iligundulika kuwa alitoroshwa na Rashid.
“Binti alitoroka kwao Nshambya na kuelekea eneo la Nyakanyasi, huko ndiko alikounguzwa kwa kumwagiwa maji ya moto,” alisema Kamanda Ollomi.
Binti huyo aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, inadaiwa alimwagiwa maji ya moto na mwanamke aliyedai ana mahusiano na mumewe.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
Post a Comment