
Ukiwa mtu wa kuangalia mambo kwa juu juu basi kila kitu kwako kitakuwa kigumu. Kusoma unaweza kuona ni kugumu, kufanya kazi kugumu, hata kusubiri mshahara unaweza kuona ni kugumu.Urahisi kwako unaweza kuwa katika kutumia pesa, pengine na kula tu. Ila watu waerevu na wenye uvumilivu kwako kila kitu kinaweza kuwa tofauti na wewe.1. Unachoona kigumu kwao wanahisi si ugumu bali ni changamoto...