Umeshaiona ndege ndefu kuliko zote duniani | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Monday, March 21, 2016

Umeshaiona ndege ndefu kuliko zote duniani

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Picha mpya za ndege ndefu zaidi duniani zimetolewa kabla ya kuzinduliwa kwa mara ya kwanza.  Ndege hiyo inayojulikana kama (The Airlander 10) ina urefu wa mita 92 ikiwa ni mita 18 zaidi ya urefu wa ndege ya kawaida.
  Kampuni moja ya uingereza imechukua miaka 9 kuijenga ndege hiyo katika kiwanda kikubwa zaidi cha ndege cha Cardington kilicho eneo la Bedfordshire  Itaondolewa kwenye kiwanda hicho kwa mara ya kwanza tangu ujenzi wake ukamilike siku ya Jumatatu.  Ndege hiyo iliyogharimu dola milioni 25 kuijenga inaweza kusimama eneo moja hewani kwa wiki tatu na na pia inaweza kuendelea kuruka hata baada ya kutobolewa mashimo kwa njia ya risasi. 
Jeshi la Uingereza liliishiwa na pesa za kumaliza ujenzi wake kuitumia kama ndege yao ya ujasusi hali iliyosababisha kampuni ya huduma za ndege ya Uingereza kujitwika jukumu la kuikamilisha.  Wengi wanaamini kuwa ndege hiyo isiyo na kelele ikiwa angani wa isiyotoa hewa chafu inaweza kutumiwa kwa usafiri siku za usoni.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA