15 wahamishiwa wizarani, watano wa hifadhi ya Ngorongoro wasimamishwa kazi na waziri Maghembe | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Friday, March 4, 2016

15 wahamishiwa wizarani, watano wa hifadhi ya Ngorongoro wasimamishwa kazi na waziri Maghembe

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Waziri wa Maliasili na Utalii  Mh.Profesa Jumanne Maghembe amewasimamisha kazi watumishi watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kuwahamisha wengine 15 kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha na ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa Umma.

Mh.waziri Maghembe amechukua hatua hiyo baada ya  kutembelea na kukutana na wafanyakazi wa mamlaka hiyo na amesema hatua zingine zitafuata kwa watumishi hao ambao wote watano ni wa idara ya uhasibu.
Kuhusu  watumishi wanaohamishwa ambao ni wa idara mbalimbali ikiwemo uhandisi,utalii na ikolojia Mh.Prof.Maghembe amesema hatua hiyo inalenga kutoa nafasi ya kuendelea  kufanyika kwa uchunguzi zaidi juu ya tuhuma mbali mbali zinazowakabili.
Mhifadhi wa Mamlaka ya Ngorongoro Bw.Fredy Manongi pamoja na kukiri kuwa mamlaka inakabiliwa na changamoto mbalimbali amesema kwa sasa tatizo kubwa ni ujangili unaofanyika katika maeneo ya mipakani japo amesema wanaendelea kuzikabili.

Hii ni ziara ya kwanza ya Waziri wa Maliasili na Utalii Jumanne Maghembe katika mamlaka hiyo ambayo amesema ni mwendelezo wa utekelezaji wa azma ya serikali ya kuimarisha uwajibikaji,ukusanyaji wa mapato na kuimarisha  shughuli za uhifadhi.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA