Said Fella kugombea urais wa Tanzania mwaka 2040 | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Friday, March 4, 2016

Said Fella kugombea urais wa Tanzania mwaka 2040

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Meneja wa Yamoto Band na TMK Wanaume Family Said Fella ‘Mkubwa Fella’ anajipanga kuogombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2040 akiwa na umri wa miaka 60.
Fella ambaye pia ni Diwani wa kata ya Kilungule wilayani Temeke jijini Dar es salaam (CCM), amekiambia kipindi cha Enewz cha East Africa Television Jumatano hii kuwa  yeye ni mtu makini,  hivyo hawezi kushindwa kuiongoza nchi.
“Kama Mungu akinipa uhai mwaka huo nitakuwa na miaka 60 na nitakuwa nina uelewa wa kutosha na uwezo wa kuweza kuwaongoza watanzania kwa kujali maslahi yao ili kuwawezesha kujikwamua na umaskini” Alisema Fella.
Aidha Fella ametamba kuwa yeye anafanya kazi kwa vitendo ndiyo maana wananchi wa kata yake walimuamini na katika madiwani wote wa Dar es salaam yeye ndiye diwani pekee aliyeshinda kwa asilimia 89% katika uchaguzi mkuu wa October 2015
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA