Watu wawili wauawa katika machafuko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Tuesday, March 8, 2016

Watu wawili wauawa katika machafuko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Watu wawili wauawa katika machafuko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Watu wawili wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika machafuko yaliyotokea kwenye eneo la Durba mkoani Haut Uélé kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Ripoti kutoka mkoani Haut Uélé zinaeleza kuwa machafuko na mapigano yalizuka wakati vijana kadhaa wanachama wa muungano wa vijana wa eneo la Durba walipokuwa wakiandamana wakidai kupatiwa maeneo ya uchimbaji madini ya dhahabu kama walivyokuwa wameahidiwa na viongozi wa serikali.
Odon Buleri, mkuu ya asasi ya kiraia katika eneo la Durba amesema kabla ya uingiliaji kati wa polisi kwa lengo la kuawatawanya waandamanaji, maandamano hayo yalikuwa yakiendelea katika mazingira ya amani. Kwa mujibu wa Buleri, awali vikosi vya polisi na jeshi la serikali vilifyatua risasi hewani na hatimaye kuwalenga waandamanaji na kusababisha vijana wawili kuuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Waandamanaji nao waliwashambulia askari kwa mawe kujibu ufyatuaji riasi huo uliofanywa dhidi yao.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA