Leo katika historia jumapili ya tarehe 03/04/2016 | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Sunday, April 3, 2016

Leo katika historia jumapili ya tarehe 03/04/2016

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

JE WAJUA? kuwa ngamia huwa anazaliwa akiwa hana nundu mgongoni? na je wajua? kuwa mtoto wa kiboko huzaliwa ndani ya maji?
Na siku kama ya leo miaka 32 iliyopita yaani mwaka 1984 kocha John Thompson wa chuo kikuu cha Georgetown cha marekani awa kocha wa kwanza mweusi kushinda shindano la mpira wa kikapu katika ligi ya NCAA.Kwa sasa ni mtangazaji wa TV na Radio katika vipindi vya michezo.
Siku kama ya leo mwaka 1862 biashara ya utumwa yapigwa marufuku Washington, D.C.
Siku kama ya leo miaka 75 iliyopita, mji wa Baghdad ulikombolewa na Rashid A'li Gilani kiongozi wa mrengo uliokuwa ukiwapinga Waingereza, baada ya mapigano yaliyotokea kati ya wazalendo waliokuwa na uchungu wa nchi yao dhidi ya serikali ya London. Gilani alikuwa akiungwa mkono na Ujerumani na kutokana na kutopata misaada kwa wakati mwafaka, vikosi vya majeshi ya Uingereza vilifanikiwa kuwakandamiza wafuasi wake. Baada ya tukio hilo serikali ya Iraq ilijiunga na nchi waitifaki katika Vita vya Pili vya Dunia.
Siku kama ya leo miaka 1007 iliyopita alifariki dunia Ibn Haytham, mwanafizikia, mwanahisabati na mwanazuoni mkubwa katika mji wa Cairo.Bwana Haytham alizaliwa mwaka 354 katika mji wa Basra kusini mwa Iraq. Alibobea katika elimu za fizikia, tiba, falsafa na unajimu. Mwanazuoni huyo ameandika vitabu vingi vya hisabati, nujumu na tiba.Moja ya vitabu vyake muhimu ni al-Manadhir ambacho kimetafsiriwa katika lugha ya Kiingereza na kinatumika katika elimu ya nujumu.

Unasemaje kuhusu hii?

KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA