Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Adam Johnson anakaribia kusomewa hukumu yake ambayo inaweza kumfanya akae jela kwa miaka isiyopungua 10. Sasa hivi ameshatoswa na club yake ya Sunderland hivvyo basi anaingia jela akiwa na machungu mara mbili.
Ikiwa imebaki kama wiki moja hadi asomewe hukumu yake Adam Johnson amefanya party kubwa usiku nyumbani kwake ambayo ilihudhuriwa na watu mbalimbali.
Kutokana na kesi yake na masharti aliyopewa haruhusiwi kutoka nyumbani muda wa usiku, hivyo basi kama anataka kufanya starehe zake zote inabidi azifanyie nyumbani.
Party hiyo ambayo ilihudhuriwa na marafiki ilifanyika kwenye nyumba yake yenye thamani ya £1.5million huko Castle Eden County Durham. Asubui mida ya saa 4 kuna picha ambazo zilipigwa za mdada mmoja akitoka kwenye party hiyo yupo chakari na chupa ya bia mkononi akitoka kwenye party hiyo.
Msichana huyo alikua hajiwezi kutokana na hangover alizokua nazo na bado anaendelea kujiongezea. Baba yake Johnson alienda kuwafungulia geti ambapo msichana huyo na mvulana mmoja waliondoka pamoja.
Adam Johnson atahukumiwa baada ya kukutwa na hatia ya kujihusisha na mapenzi na msichana mwenye miaka 15. Adam alimshawishi msichana huyo kupitia messenger ya Whatsapp.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment