Ajuza aliyemualika Obama apata majibu Cuba | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Saturday, March 19, 2016

Ajuza aliyemualika Obama apata majibu Cuba

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Mwanamke mmoja aliyemwalika rais wa Marekani Barrack Obama nyumbani kwake nchini Cuba amepokea majibu kutoka kwa rais huyo baada ya mawasiliano ya moja kwa moja kati ya Marekani na Cuba kurejeshwa.
Ileana Yarza,mwenye umri wa miaka 76 aliandika kwa rais Obama mnamo mwezi Februari akimkaribisha kwa kikombe cha kahawa nyumbani kwake huko Havana.
Barua hiyo inayompatia asante bi Yarza ilipelekwa nchini Cuba siku ya Jumatano.
Zilikuwa barua za kwanza kuwasili nchini Cuba kutoka Marekani baada ya kipindi cha miaka 50.
Mawasiliano ya kutuma ujumbe wa moja kwa moja kati ya mataifa hayo mawili yalikatizwa wakati wa vita baridi,huku barua zilizoandikwa zikipitia mataifa mengine kama vile Mexico na Canada.
Bi Yarza aliandika kwa Obama mnamo tarehe 18 mwezi Februari baada ya kugundua kwamba anajiandaa kuizuru Cuba mnamo mwezi Machi,akimwabia:Raia wa Cuba ambao wangependelea kukutana nawe kibinafsi ni wachache.
Rais Obama alimshukuru Bi Yarza kwa usaidizi wake akiongezea kuwa barua hiyo ni ishara ya uhusiano mzuri katika siku za usoni kati ya mataifa hayo mawili.
Na hakumpuuza kuhusu kikombe cha chai akisema kuwa atatafuta muda.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA