Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Waziri mkuu wa Cambodia amekana kununua 'likes' bandia za ukurasa wake wa facebook ,baada ya kiongozi wa upinzani kumshtumu kwa kuongeza umaarufu wake.
Hun Sen mwenye umri wa miaka 63,anayejiita gwiji wa teknolojia huchapisha mara kwa mara kuhusu maisha yake katika mtandao wake.
Ukurusa wake ulioanza mwezi Septemba una takriban 'likes' milioni 3.2.
Wiki iliopita,iliripotiwa kuwa 'Likes' zake nyingi zinatoka katika akaunti za kigeni.
'Likes' nyingi zilitoka kutoka kwa akaunti za nchi za India {255,692} huku nyengine zipatazo {98,256}zikitoka Ufilipino,{46,368} zikitoka Myanmar na {46,368} zikitoka Indonesia na maeneo mengine.
''Nimetambuliwa na raia wa India''.
Huku kukiwa na upinzani mkali,Hun Sen na kiongozi wa upinzani Sam Rainsy anayeishi ugenini ni washindani wakuu katika mitandao.
Wote wana matumaini ya kushinda idadi kubwa ya wapiga kura ambao mwaka 2013 walimpigia kura bwana Rainsy wa chama cha Cambodia National Rescue Party {CNRP} katika uchaguzi ambao wanasema ulikumbwa na udanganyifu.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment