BINTI MUUZA DUKA AMPAGAWISHA MAYWEATHER, SASA WANAKULA BATA KWENDA MBELE | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Monday, March 14, 2016

BINTI MUUZA DUKA AMPAGAWISHA MAYWEATHER, SASA WANAKULA BATA KWENDA MBELE

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Maisha yanaweza kubadilika mara moja tu bila ya wewe kutarajia, ndivyo ilivyo mtokea binti aitwaye Rmarni Ellis, mwenye umri wa miaka 19 tu.

Yeye alikuwa mfanyakazi wa duka moja jijini London, bahati yake ikaanzia pale bondia maarufu na mwanamichezo tajiri kuliko wote duniani, Floyd Mayweather alipoingia pale.

Wakati akipata huduma, Mayweather akaonekana kuvutiwa na binti huyo. Mwisho “akachombeza” na sasa Rmarni yuko jijini Miami, Marekani.


Huko amekuwa akionekana akila raha pamoja na Mayweather na hakuna ubishi tena kwamba sasa ni wapenzi.

Wawili hao wamekuwa wakionekana wakila bata kupitia mtandao wa Instagram wa binti huyo.


Mkali huyo wa masumbwi anaonekana amefika kabisa kwani yuko huru kuonekana akijiachia na binti huyo.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA