ISIS inatenda 'jinai za kivita, jinai dhidi ya binadamu' | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Wednesday, March 16, 2016

ISIS inatenda 'jinai za kivita, jinai dhidi ya binadamu'

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
ISIS inatenda 'jinai za kivita, jinai dhidi ya binadamu'
Wabunge nchini Marekani wamepitisha azimio la kutangaza kundi la kigaidi la Daesh au ISIS kuwa linatekeleza mauaji ya kimbari nchini Iraq na Syria.
Katika azimio lililopitishwa kwa kauli moja Jumatatu, serikali ya Rais Barack Obama imetakiwa kutangaza kuwa jinai zinazotekelezwa na ISIS ni 'jinai za kivita, jinai dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari.
Bunge la Wawakilishi Marekani limeptisha azimio hilo katika hali ambayo magaidi wa ISIS walipata mafunzo yao ya kwanza mwaka 2012 nchini Jordan chini ya usimamizi wa Shirika Ujasusi la Marekani CIA kwa lengo la kuiangusha serikali ya Syria. Hivi sasa magaidi hao wanadhibiti baadhi ya maeneo ya Iraq na Syria.
Magaidi hao wamekuwa wakitekeleza vitendo vya kikatili dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Sunni, Shia na pia Wakurdi wa pote la Izadi na Wakristo katika maeneo wanayoyadhibiti.
Marekani na waitifaki wake wamehusika katika uanzishaji makundi ya kigaidi kama vile Al Qaeda na ISIS na kisha kushindwa kidhahiri kuyadhibiti makundi hayo ambayo sasa yanatekeleza jinai za kutisha kote duniani.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA