Saudi Arabia kuwaachisha kazi Wayemeni 35 elfu | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Wednesday, March 16, 2016

Saudi Arabia kuwaachisha kazi Wayemeni 35 elfu

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Saudi Arabia kuwaachisha kazi Wayemeni 35 elfu
Saudi Arabia imesema kuwa karibuni hivi itawafuta kazi raia wa Yemen wapatao 35 elfu wanaofanya kazi nchini humo.
Vyombo vya habari vya Yemen vimeripoti kuwa, utawala wa Aal-Saud umeamua kuchukua hatua hiyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi unaoukumba kwa sasa. Habari zinasema kuwa, aghalabu ya raia hao ambao watapigwa kalamu nyekundu na watawala wa Riyadh ni wafanyakazi katika sekta ya simu za rununu. Raia hao wa Yemen ambao wanategemewa na zaidi ya familia laki moja wamepewa muda wa miezi mitatu kujiuzulu la sivyo wafutwe kazi. Hii ni katika hali ambayo, uchumi wa Saudia umekuwa ukiyumba katika miezi ya hivi karibuni haswa baada ya serikali ya Riyadh kuanzisha hujuma za anga dhidi ya raia wasio na hatia nchini Yemen. Wizara ya Leba ya Saudi Arabia mnamo Machi 8 ilisema kuwa inapanga kuwafuta kazi raia wa Yemen ili kutoa nafasi za ajira kwa raia wake. Saudi Arabia ilianzisha mashambulizi ya kijeshi nchini Yemen tarehe 26 mwezi Machi mwaka jana 2015, lengo likiwa ni kuisambaratisha harakati ya Ansarullah na kumrejesha madarakani Rais mtoro wa Yemen aliyejiuzulu Abdu-Rabuh Mansour Hadi. Zaidi ya watu 8,400 wameuawa na wengine wasiopungua 16 elfu wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA