Kenya yathibitisha visa 2 vya homa ya manjano | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Friday, March 18, 2016

Kenya yathibitisha visa 2 vya homa ya manjano

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Kenya imethibitisha visa viwili vya ugonjwa wa homa ya manjano vilivyopatikana kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha miongo miwili.
Visa vyote viwili vilitoka nchini Angola ambapo mripuko wa ugonjwa huo umewauwa watu 150.
Wakenya hao 2 waliwasili na ugonjwa huo kutoka Angola ambapo wamekuwa wakiishi na kufanya kazi kwa zaidi ya miaka 10.
Mgonjwa wa kwanza alifariki siku ya Jumatano katika hospitali ya Kenyatta huku mgonjwa wa pili akiendelea kupata matibabu katika hospitali hiyo.
Maafisa wa afya wanasema wameimarisha doria yao huku wakiwahakikishia Wakenya kwamba hakuna hatari ya maambukizi ya moja kwa moja kupitia mbu.
Homa ya manjano ilikuwa imeangamizwa nchini Kenya.
Haina dawa,lakini ishara zake zinaweza kukabiliwa.
Angola inapambana na mripuko wa homa hiyo na imeanza kutoa chanjo kwa raia wake inayolenga watu milioni 7 katika eneo la Luanda lililoathirika
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA