Mchora vibonzo 'Gado' kumshtaki muajiri wake | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Thursday, March 10, 2016

Mchora vibonzo 'Gado' kumshtaki muajiri wake

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Mchoraji vibonzo wa Kenya Godfrey Mwapembwa ,aka Gado amesema kwamba atalishtaki gazeti la The daily Nation nchini Kenya kuhusu kile alichokitaja kuwa kusimamishwa kwa kandarasi yake kinyume cha sheria.
Mwaka uliopita alienda likizo kufuatia kile alichosema ni kuingiliwa kwa kazi yake.
Alikuwa amechora kibonzo katika gazeti jingine kuhusu raliyekuwa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ambacho anasema hakikumuangazia vizuri.
Mhariri wake katika gazeti hilo alipendekeza kwamba apumzike kwa kuwa sio mfanyikazi kamili wa gazeti hilo lakini amepewa kandarasi ya kuchora vibonzo hadi mwezi Julai 2016.
Hatahivyo mwezi uliopita alipewa barua ya kumsimamisha kazi.
Gazeti hilo limesisitiza kuwa uamuzi huo wa kuachana uliafikiwa na pande zote mbili,lakini mchoraji huyo anaamini kwamba kufutwa kwake kulitokana na shinikizo za kisiasa akiongezea kuwa anaamini kwamba serikali ya Uhuru Kenyatta imekuwa haipendezwi na kazi.
Mwapembwa ni mchora vibonzo maarufu nchini Kenya ambaye huwachekesha wasomaji wengi kwa uchoroji wake.
Mtandao wake unaomtaja kuwa mchoraji vibonzo hodari wa kisiasa katika eneo la mashariki na Afrika ya kati,anasema kuwa vibonzo vyake huangazia kila swala kutoka ugaidi,ukataji miti,ukimwi na ufisadi na vibonzo vyake vimekuwa vikizua mjadala mkubwa.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA