Mwanamke amsafirisha mtoto ndani ya begi | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Thursday, March 10, 2016

Mwanamke amsafirisha mtoto ndani ya begi

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Mwanamke mmoja alisafiri kwa ndege kutoka Istanbul nchini Uturuki hadi mjini Paris akiwa na mtoto aliyemficha katika begi lake la mkononi,shirika la ndege la Air Ufaransa limesema.
Shirika hilo limesema kuwa mtoto huyo aliyesafiri bila kulipa nauli alipatikana ndani ya ndege hiyo siku ya Jumatatu usiku.
Duru katika shirika hilo iliambia shirika la habari la AFP kwamba mwanamke huyo ni mkaazi wa Ufaransa ambaye alikuwa katika harakati za kumfanya mtoto huyo kutoka Haiti kuwa wake.
Shirika hilo la ndege lilielezea mamlaka ya Ufaransa lakini waendesha mashtaka wakaamua kutofungua mashtaka.
Mwanamke huyo alikuwa akingoja kuchukua ndege nyengine mjini Istanbul lakini akazuiliwa kupanda ndege hiyo na mtoto huyo ,duru hiyo iliarifu AFP.
Alinunua tiketi nyengine na kumficha mtoto huyo ndani ya begi.
Alipokuwa ndani ya ndege hiyo ,alimuweka mtoto huyo katika miguu na kujifunika na blanketi ,lakini mtoto huyo wa kike alitaka kwenda chooni na alionekana na abiria wengine.
Haijulikani mtoto huyo alikuwa na miaka mingapi ,duru moja ilieleza kwamba alikuwa na miaka minne huku nyengine ikisema alikuwa na mwka mmoja ama miwili.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA