Mfuasi wa IS akamatwa na Marekani | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Friday, March 11, 2016

Mfuasi wa IS akamatwa na Marekani

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Jeshi la Marekani limethibitisha kuwa vikosi vyake maalumu vimefanikiwa kumkamata mtalaam wa silaha za kikemikali wa kundi la wapiganaji wa Islamic State huko nchini Iraq.
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani Peter Cook, amesema kukamatwa kwa Sulayman Daoud Al Al Bakr or Abu Daoud ni kufuatia taarifa za kiintelijensia kuhusiana na kundi hilo na matumizi ya silaha za kikemikali.
Amesema kuwa taarifa hizi pia zimewezesha vikosi vya Marekani kufanikisha mashambulizi ya anga dhidi ya wapiganaji wa Islamic State.
Sulayman Daoud anasemekana kuwa alikuwa mtu wa karibu katika mpango wa matumizi ya silaha za kikemikali ambao ulianzishwa na na Saddam Hussein.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA