MSN YAISAMBARATISHA ARSENAL (Video) | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Thursday, March 17, 2016

MSN YAISAMBARATISHA ARSENAL (Video)

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
MSN
Barcelona ambao ndiyo mabingwa watetezi wa kombe la vilabu bingwa Ulaya wamefuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya kuichapa Arsenal kwa bao 3-1 kwenye mchezo wa marejeano uliochezwa kwenye uwanja wa Nou Camp.
Wakiwa wanaongoza kwa bao bao 2-0 za mchezo wa kwanza, Lionel Messi alishuhudiwa akimlazimisha David Ospina kufanya kazi ya ziada kuokoa shuti la karibu kutoka kwa nyota huyo kalba ya Neymar kupachika mpira kambani.
MSN 1
Mohamed Elneny aliisawazishia Arsenal bao hilo kipindi cha pili lakini Suarez aliongeza bao linguine na kuipa Barcelona uongozi wa bao 2-1.
Elneny
Shuti la Danny Welbeck liligonga mwamba kabla Messi hajalizamisha kwa mara nyingine jahazi la Arsenal na kuwatupa nje ya mashindano kwa kukandamiza bao la tatu kwenye mchezo huo.
Ushindi huo unamaanisha Barcelona imefuzu kwenye hatua ya nane bora kwenye mashindano hayo kwa mara ya tisa mfululizo.
MSN 2
Lakini mbali na kufuzu hatua ya robo fainali ya Champions League, Barcelona imeendeleza rekodi ya kutopoteza mchezo na kufikisha michezo 38 bila kupoteza kwenye michuano yote huku wakitafuta rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutetea ubingwa wa Ulaya.
No side has won back-to-back European Cups since AC Milan in 1989 and 1990.
MSN 4
Hakuna timu iliyofanikiwa kushinda Champions League mara mbili mfululizo tangu AC Milan ilipofanya hivyo mwaka 1989 na 1990.
Miamba hiyo ya Catalan bado ipo kwenye makombe yote msimu huu (Champions League, La Liga na Copa del Rey) huku wakiwa katika nafasi nzuri kwenye kila mashindandano.
MSN 6
Kikosi cha Luis Enrique kipo mbele kwa tofauti ya point inane kileleni mwa ligi ya Hispania zikiwa zimesalia mechi tisa na watacheza fainali ya Copa del Rey dhidi ya Seilla mwezi May.
MSN 5
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA