Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Msemaji wa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, watu 106 waliuawa na ndege za Saudia katika soko la Mastaba nchini Yemen.
Akitangaza habari hiyo hapo jana Robert Kelfer amesema kuwa, miongoni mwa wahanga wa shambulio hilo la kikatili, walikuwa ni watoto wadogo 24. Aidha Kelfer ameongeza kuwa, katika hujuma hiyo maduka 16 ya soko hilo yaliharibiwa kikamilifu na kusisitiza kuwa, Saudia ndiyo inayobeba jukumu la jinai hiyo. Msemaji wa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, amesema kuwa soko hilo lilikuwa kituo kikuu cha manunuzi kwa vijiji 15 vya mkoa wa Hajjah na kwamba ndege za Saudia zilifanya hujuma hiyo katika wakati ambao soko hilo lilikuwa limejaa watu. Saudi Arabia kwa kushirikiana na nchi kadhaa, ilianzisha mashambulizi ya kivamizi mwezi Machi mwaka jana kwa lengo la kuwashinikiza raia wa Yemen kumkubali kibaraka wake Abd Rabbuh Mansur Hadi, aliyekuwa rais wa nchi hiyo na aliyetangaza kujiuzulu na kukimbilia Saudia. Hata hivyo hujuma hizo hazijafanikiwa kutokana na Wayemen kuendelea kusimama imara dhidi ya njama hizo chafu za Saudia.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment