Al-Shabab washambulia Kismayo, watatu wauawa | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Sunday, March 20, 2016

Al-Shabab washambulia Kismayo, watatu wauawa

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Al-Shabab washambulia Kismayo,  watatu wauawa
Watu watatu wameripotiwa kuuawa na wengine sita kujeruhiwa kufuatia shambulio lililofanywa na kundi la kigaidi la ash-Shabab katika eneo lililoko karibu na mji wa Kismayo nchini Somalia.
Shambulio hilo limehusu kiwanda cha makaa ya mawe cha eneo la Burjabu lililoko umbali wa kilometa 40 magharibi mwa mji wa Kismayo. Kwa mujibu wa mashuhuda, wahanga wa shambulio hilo ni wafanyakazi wa kiwanda hicho, na kwamba walikumbwa na hujuma hiyo wakati walipokuwa wakikata miti katika eneo hilo. Habari zinasema kuwa, wanamgambo wa kundi hilo la kitakfiri walikuwa wakiingiza pato kubwa la fedha kutokana na biashara ya makaa ya mawe katika mji wa Kismayo wenye umuhimu mkubwa baada ya mji mkuu wa Somalia, Mogadishu. Ni vyema kuashiria kuwa, licha ya kundi la ash Shabab kufurushwa kutoka katika miji muhimu ya nchi hiyo, lakini linaendelea kufanya mashambulizi katika maeneo tofauti ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA