Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa ripoti kuhusu mgogoro wa maji na hatari ya kuchafuliwa kwa maji kote duniani.
Katika ripoti hiyo WHO imesema kuwa, katika kila dakika mbili mtoto mmoja hukabiliwa na hatari ya kufariki dunia kutokana na kunywa maji machafu. Ripoti hiyo imesema kuwa, asilimia 10 ya watu duniani hawapati maji safi ya kunywa na kwa msingi huo wanakabiliwa na hatari ya maradhi ya tumbo na kufariki dunia.
Shirika la Afya Duniani limesema dola moja inayotumiwa kwa jili ya kudhamini maji safi ya kunywa na huduma za maji taka inaweza kuokoa hasara ya dola nne hadi 11. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, kutokana kukaribia Siku ya Kimataifa ya Maji hapo Jumanne ijayo, WHO inafanya jitihada kuelekeza macho ya walimwengu kwenye maudhui hii hususan uhusiano uliopo baina ya maji na ajira na msaada wake katika uchumi unaozingatia mazingira.
Wakati huo huo Shirika la Watoto Duniani (UNICEF) limetahadharisha kuwa, kutokuwepo maendeleo ya kutosha katika suala la kudhibiti maji taka kunayafanya maisha ya watoto yakabiliwe moja kwa moja na hatari kubwa.
Ripoti ya Shirika la Afya Duniani inasema kuwa kila siku watu elfu 30 hufariki dunia kutokana na kukosa maji safi na salama ya kunywa. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, asilimia 80 ya magonjwa yanayowasumbua wanadamu duniani yanatokana na ukosefu wa maji ya kutosha.
Machi mwaka jana Umoja wa Mataifa ulitoa ripoti ukitahadharisha kwamba, kama hakutafanyika mageuzi basi dunia itakumbwa na mgogoro wa maji ambao utakuwa na taathira kubwa na mbaya sana kwa nchi zenye joto na uhaba wa maji. Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imesisitiza kuwa maji yanafujwa na kutumiwa vibaya katika maeneo mblimbali duniani kwa kadiri kwamba kwa mwenendo huu wa sasa, hadi kufikia mwaka 2030 dunia itakumbwa na uhaba wa asilimia 40 ya maji.
Ripoti ya kila mwaka kuhusu maji imesema kuwa dunia ina maji ya kutosha ya kukidhi mahitaji ya walimwengu wote lakini kuna ulazima wa kufanyika mabadiliko katika utumiaji, mbinu za usimamizi na ugavi wa maji. Ripoti hiyo pia imesisitiza udharura wa kuwepo usimamizi mzuri wa vyanzo vya maji.
Ripoti hiyo inasema kuwa, ukuaji wa idadi ya watu ni miongoni mwa sababu kuu za mgogoro wa sasa wa maji kote duniani. Jamii ya karibu watu bilioni 7 na milioni 300 duniani kila mwaka inaongezeka kwa karibu watu milioni 80. Kwa utaratibu huo kuna uwezekano kwamba, hadi kufikia mwaka 2050 idadi ya watu duniani itafikia karibu bilioni 9 na milioni 100. Ili kuweza kukidhi mahitaji ya chakula ya watu hao uzalishaji wa sekta ya kilimo- ambao kwa sasa unatumia asilimia 70 ya maji yote ya dunia-, unapaswa kustawi na kuongezeka kwa asilimia 60.
Zaidi ya nusu ya watu duniani wanadhamini mahitaji yao ya maji ya kunywa kutoka kwenye vyanzo vya chini ya ardhi. Wakati huo huo asilimia 43 ya maji yote yanayotumika duniani kwa ajili ya kilimo cha kunyunyizia yanatokana pia na maji ya chini ya ardhi. Kwa msingi huo ripoti zinasema kuwa, karibu asilimia 20 ya maji ya chini ya ardhi yanakaribia kukauka kutokana na kutumiwa kupita kiasi. Mabadiliko ya hali ya hewa yaliyoathiri kiwango cha maji ya mvua, wakati na meneo inakonyesha, na idadi kubwa ya watu kuhamia maeneo ya mijini pia vimezidisha mgogoro wa maji duniani. Tunaongeza kuwa watafiti wa Chuo Kikuu cha Colorado huko Marekani wamesema kuwa akiba ya maji ya kunywa ya dunia inapungua kila mwaka na kwamba hadi miaka 25 ijayo dunia itakumbwa na tatizo la uhaba wa maji.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment