Traffic ndani ya siku 12 wakusanya milioni 577 za makosa barabarani na kigogo wa madawa ya kulevya mwingine atiwa mbaroni | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Saturday, March 19, 2016

Traffic ndani ya siku 12 wakusanya milioni 577 za makosa barabarani na kigogo wa madawa ya kulevya mwingine atiwa mbaroni

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam inawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroine zenye uzito wa kilo moja, akiwamo anayedaiwa kuwa kigogo wa biashara ya dawa hizo nchini.
Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, juzi saa 1.15 usiku katika maeneo ya Mbezi Beach, walimkamata mtuhumiwa wa kwanza akiwa na gari baada ya kumpekua alikutwa na dawa hizo za kulevya.
Alisema walipomhoji zaidi, alidai kuwa dawa hizo siyo zake, bali za tajiri yake anayeishi Mikocheni jijini hapa ambaye wali panga kukutana naye maeneo ya Mbezi Beach kwa ajili ya kukabidhiana.
Alisema upelelezi unaendelea na utakapokamilika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
Kukamatwa kwa kigogo huyo na msaidizi wake ni mafanikio ya jeshi hilo ambalo hivi karibuni lilimkamata kigogo mwingine muuza ‘unga’ jijini hapa hivi karibuni.
Wakati huohuo,Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kupitia kitengo chake cha usalama Barabarani limekamata magari mbalimbali kwa makosa ya usalama barabarani
Jumla ya Tshs. 577,831,000 zimekusanywa ikiwa ni tozo kwa makosa hayo kwa mida wa siku 12, kuanzia 07/03/2016 hadi tarehe 18/03.2016.
Kamanda Sirro amewataka madereva kuwa makini na waangalifu pindi wawapo barabarani ili kuepuka adhabu zitolewazo ili vipato hivyo viwasaidie katika maisha yao ya kila siku.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA