Vurugu kabla ya uchaguzi zinachafua usalama Zambia | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Sunday, March 20, 2016

Vurugu kabla ya uchaguzi zinachafua usalama Zambia

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Vurugu kabla ya uchaguzi zinachafua usalama Zambia
Rais wa Zamani nchini Zambia, Kenneth Kaunda amesema kuwa, vurugu za kisiasa ambazo zimekuwa zikitokea katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi wa mwezi Agosti mwaka huu, zinaathiri usalama wa nchi hiyo.
Kaunda aliyeyasema hayo wakati akizungumza katika kikao kilichopewa jina la mhimili wa amani, amewataka wadau wa kisiasa na viongozi wa Tume ya Uchaguzi nchini Zambia kufanya mazungumzo ya kutatua matatizo hayo ya kisiasa. Ameongeza kuwa, hiyo ndio njia pekee itakayosaidia kuimarisha usalama na amani nchini humo. Aidha rais huyo wa zamani wa Zamabia ameyataka makundi tofauti ya kisiasa kuheshimiana, hususan wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Agosti. Migogoro ya kisiasa nchini Zambia imeshika katika katika hali ambayo nchi hiyo inajiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa rais, bunge na madiwani uliopangwa kufanyika tarehe 11 mwezi Agosti mwaka huu. Kenneth Kaunda alikuwa rais wa Zambia kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1991.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA