Wafanya ziara wazidi kuandamwa na ajali Saudia | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Sunday, March 20, 2016

Wafanya ziara wazidi kuandamwa na ajali Saudia

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Wafanya ziara wazidi kuandamwa na ajali Saudia
Huku ulimwengu ukiwa bado haujasahau vifo vya kutisha vya maelfu ya mahujaji wa nyumba ya Mwenyezi Mungu nchini Saudia, wafanya umra wapatao 19, wamepoteza maisha katika ajali nyingine mbaya ya basi nchini humo.
Kwa mujibu wa duru za habari nchini Saudia, wafanya ziara hao raia wa Misri wamefariki dunia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupinduka. Basi hilo ambalo lilikuwa limebeba wafanya umra wapatao 44 wote kutoka Misri wakiwamo watoto wawili, lilipata ajali kati ya mji mtukufu wa Makkah na Madina. Watu wengine 22 wamejeruhiwa baadhi yao wakiwa na hali mbaya. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana, ingawa ripoti za awali zinaeleza kuwa ni dereva kuzidiwa na usingizi. Hisham al Naqib, mmoja wa viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje nchini Misri amenukuliwa akisema kuwa, miili ya wahanga wa ajali hiyo iko hospitalini mjini Madina. Kwa upande wake, Nawaf al-Muhammad, mkuu wa idara ya usafirishaji ya mjini Madina amesema kuwa, kuna uwezekano mkubwa kwamba dereva alizidiwa na usingizi. Hii ni katika hali ambayo Ijumaa iliyopita, wafanya ziara 14 raia wa Palestina walifariki dunia katika ajali nyingine ya barabarani mjini Makka, Saudia. Vifo hivyo vinatokea katika hali ambayo hadi sasa ulimwengu wa Kiislamu unaendelea kuilalamikia Saudia juu ya uzembe wake katika kusimamia ibada ya Hija na kuitaka Riyadh ikabidhi jukumu hilo kwa nchi za Kiislamu.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA