Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Wakati Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, akidai wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wanakamatwa bila sababu za msingi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, amaesema hakuna mtu anayekamatwa bila sababu na kwamba yeyote atakayebainika kufanya kosa, atasweka ndani bila kujali chama chake.
Machi Mosi, mwaka huu, Mbowe aliwaeleza waandishi wa habari kwamba wabunge na madiwani kutoka Ukawa, wanadhalilishwa na kunyanyaswa kila kona nchini na kwamba hizo ni juhudi za kurudisha nyuma maendeleo ya kazi za viongozi hao.
Hivi karibuni, Waziri Kitwanga alisema kuwa wananchi watambue kwamba askari polisi ni rafiki wa raia mwema, hivyo hawawezi kumkamata mtu asiyetenda kosa.
“Nitamshangaa askari polisi, mtu anatenda kosa pale wasimkamate eti kwa sababu tu ni mbunge wa upinzani. Awe wa CCM, awe wa upinzani watakamatwa, mimi nimeshawaeleza.
“Nimeshawaeleza wazi kabisa, mimi nitasimamia haki tu, tofauti na hapo hapana, wewe ungeona yule mama alivyopigwa na wabunge(Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando) inaumiza sana. Nilichukia sana lakini hata sikuwasemesha polisi, nilikaa kimiya tu niwaone watafanyaje.
“Niliamua kuwapima, ‘infact’ (kwa kweli) hawa watu hata dhamana wasingewapa kwa kitendo hicho,” alisema Kitwanga.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment