Wapiganaji wa al-Shabaab wazingirwa Somalia | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Friday, March 18, 2016

Wapiganaji wa al-Shabaab wazingirwa Somalia

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Wapiganaji takriban 200 waliokuwa wameshambulia eneo moja katika jimbo la Puntland, wamezingira na wanajeshi wa jimbo hilo.
Naibu rais wa jimbo hilo Abdihakim Amry amesema kwamba wanajeshi hao wamewapa wapiganaji hao agizo la kuwataka kujisalimisha la sivyo wakabiliwe.
Mapigano makali yamekuwa yakiendelea katika eneo hilo la Suuj, ambalo linapatikana katika mkoa wa Nugaal katika pwani ya jimbo hilo lililo na uhuru kiasi kutoka kwa Somalia.
    Wapiganaji 30 wa al-Shabab wauawa Somalia
Wapiganaji wa al-Shabaab walifika eneo hilo kwa boti na kuchukua udhibiti.
Wanajeshi watano wa Puntland wanaripotiwa kuuawa kwenye mapigano na wanamgambo hao katika eneo hilo.
Jana, kituo cha redio cha kibinafsi cha Radio Mustaqbal kilimnukuu Naibu Waziri Mkuu wa Somalia Mohamed Omar Arte akisema serikali kuu iko tayari kutuma wanajeshi wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika (Amisom) “kukabiliana na wapiganaji hao wa al-Shabab eneo la Puntland iwapo watahitajika”.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA