Wavuliwa nguo hadharani kisa "vimini" Mbeya | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Friday, March 11, 2016

Wavuliwa nguo hadharani kisa "vimini" Mbeya

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

Wasichana wanaovaa nguo fupi za kubana na wavulana wanaovaa milegezo  jijini Mbeya , juzi walipata wakati mgumu baada kundi la vijana kuwavua nguo zao na kuzichana hadharani, kutokana na gari la matangazo kupita jijini hapa likiwataka watu kuvaa nguo za heshima zinazoendana na maeneo husika.
Tangu Machi 7 hadi 9, gari la matangazo ya Kampuni ya Studio H ya Huruma lilipita mitaa mbalimbali ya jijini Mbeya, likiwataka wasichana kuacha kuvaa vimini na vijana kuacha kuvaa mlegezo.
Baada ya tangazo hilo, vijana walianza kuwavamia wasichana na wavulana waliovaa milegezo maeneo ya Uyole, Soweto, Kabwe na Mwanjelwa, huku wanawake waliokuwa wakiuza matunda wakiwarushia vitenge wasichana waliochaniwa nguo ili wajisitiri.
Ofisa Habari Jiji la Mbeya, John Kilua alisema uongozi hauhusiki na tangazo hilo.
Hata hivyo, Ofisa wa Kampuni ya Studio H ya Huruma, Siyata Mbua alisema walitoa tangazo hilo baada ya kukamilika kwa makubaliano baina ya jiji na kampuni yake.
Mbua alisema kazi ya kuzuia nguo zisizo za heshma inahusu Serikali, lakini kampuni iliamua kujitolea kwa makubaliano na jiji kwa mwaka mmoja.
“Lengo ni kuwahamasisha wananchi wavae nguzo za heshima. Hatuwahamasishi vijana wawavamie watu, bali tunawataka kila mmoja avae nguo kulingana na maeneo anayofanyia kazi,”alisema. Mabua alisema lengo ni kuelimishana zaidi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema hajapata malalamiko na kuwataka vijana kuheshimu utu wao kwa kuvaa nguo za heshima.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA