WIzara yafunguka na kusema haya kuhusu filamu iliyompatia tuzo Elizabeth Michael "Lulu" | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Thursday, March 17, 2016

WIzara yafunguka na kusema haya kuhusu filamu iliyompatia tuzo Elizabeth Michael "Lulu"

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kumekuwa na minongono mingi kutoka kwa baadhi ya wananchi kuhusu Filamu ya Mapenzi ya Mungu ya msanii Elizabeth Michael (Lulu) iliyoshinda tuzo ya Filamu bora Afrika Mashariki mapema mwezi huu huko Lagos Nchini Nigeria katika tuzo za African Magic Views Choice Award (AMVCA).
Ili filamu ikamilike inahusisha watu mbalimbali wanaoshirikishwa kukamilisha filamu kuanzia mtoa wazo ambaye wazo hilo huwekwa katika mswada na mtaalamu jambo ambalo haliondoshi umiliki wa filamu.
Tunapenda kuufahamisha umma kuwa mmiliki halali wa Filamu ya Mapenzi ya Mungu ni Msanii Elizabeth Michael (Lulu) na ndiye aliyepata tuzo kwani ana haki zote za kupata tuzo hiyo kama mmiliki halali wa filamu hiyo.
Filamu ya Mapenzi ya Mungu imetengenezwa chini ya kampuni ya Proin Promotion na imesajiliwa kwa namba ya usajili CO831190.
IMETOLEWA NA
WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA