Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Manchester United imeendelea kutekeleza sera yake ya kuwekeza kwa vijana baada ya mashetani hao wekundu kufanikiwa kumsajilikinda wa miaka 16 Nishan Burkhart kutoka klabu ya FC Zurich.
Story hiyo imethibitishwa na gazeti la kilasiku la Blick la Uswiss ambalo linapicha pamoja nukuu za kuthibitisha uhamisho huo.
Picha hiyo inamuonesha Burkhart ambaye anacheza nafasi ya ushambulizi akiwa na wazazi wake pamoja na kocha msaidizi wa Man United Ryan Giggs.
Baba wa kinda huyo Stefan Burkhart, ameliambia Blick: Tumeamua kuachana na klabu hii wakati wa majira ya joto. Nishan anahamia Manchester United, anamawazo tofauti.
Je, huyu ni Marcus Rashford mwingine?
Nishan Burkhart ni mshambuliaji wa kati amabye amejizolea umaarufu hasa kwa uwezo wake mkubwa wa mguu wa kulia.
Anatarajiwa kujiunga na academy ya Man United na kuandaliwa kuingia kwenye timu ya vijana mara atakapotua Carrington.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment