Jiji la Dar es Salaam Kufumuliwa na Kupangwa Upya | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Saturday, April 16, 2016

Jiji la Dar es Salaam Kufumuliwa na Kupangwa Upya

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

 Waziri wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema Jiji la Dar es Salaam litafumuliwa na kupangwa upya baada ya Ramani ya Mipango Miji (Master Plan) mpya kukamilika.  Pia, amesema Serikali ipo kwenye mkakati wa kuhakikisha ndani ya miaka 10 ijayo, ardhi yote nchini itakuwa imekamilika kupimwa na kupangwa kwa matumizi mbalimbali.   Akizungumza na wadau wa Sekta ya Uendelezaji Ujenzi Dar es Salaam jana, Waziri Lukuvi alisema Jiji la Dar es Salaam linaongoza kwa ubovu wa upangaji miji.
   Alisema kwa sababu hiyo, ameagiza kuandaliwa kwa Mpango Mji Mpya ambao utakamilika Julai, baada ya ule wa awali kuoneakana mbovu.   “Mwanzo hatukufanya vizuri. Tuliajiri Consultant (mshauri) wa Master Plan (Mipango Miji) kutoka Italia sitaki kumtaja na yule Mswahili na wengine walioshirikiana nao, lakini kwa ufupi walifanya vibaya. Fedha imekwisha lakini kazi siyo nzuri,” alisema.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA