Leo katika historia jumamosi ya tarehe 16/04/2016 | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Saturday, April 16, 2016

Leo katika historia jumamosi ya tarehe 16/04/2016

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja

JE WAJUA? kuwa unyevu ndio unaosababisha gundi aina ya super glue kuganda na sio hewa?
Siku kama ya leo miaka 19 iliyopita ulitokea mlipuko mkubwa ulisababishwa na mtungi wa gesi na kusambaza moto kwenye mahema ya Mahujaji huko Mina kilomita 10 kutoka katika mji wa Mtakatifu wa Makka. Mahujaji wasiopungua 343 walifariki dunia na wengine 1,290 kujeruhiwa katika tukio hilo. Aidha mahema yasiyopungua elfu sabini yaliteketea kwa moto huo. Hilo linahesabiwa kuwa tukio kubwa la pili la janga la moto kutokea wakati wa msimu wa Hija. Mnamo mwaka 1975, ulitokea moto mkubwa huko Mina nchini Saudi Arabia uliosababisha vifo vya maelfu ya Mahujaji na wengine wengi kujeruhiwa. Kutokana na matukio hayo, Saudi Arabia ililazimika kuweka katika eneo la Mina, mahema yasiyoshika moto ili kuepusha ajali za moto.
Na miaka 127 iliyopita, Charles Spencer Chaplin mcheza filamu na msanii mashuhuri wa tasnia ya filamu alizaliwa katika viunga vya mji wa London  Uingereza. Alipokuwa mdogo, alianza na michezo ya kuigiza na kupata umashuhuri hatua kwa hatua. Mwanzoni mwa ujana wake, Chaplin alielekea nchini Marekani kwa lengo la kutengeneza filamu. Lakini kutokana na kutengeneza filamu ya ukosoaji na yenye kuonyesha mshikamano wake na matabaka ya kimasikini katika jamii ya Marekani, serikali ya nchi hiyo ilitoa amri ya kubaidishwa kwake mnamo mwaka 1952. Chaplin alikumbana na mazingira magumu ya kufanya shughuli zake nchini Marekani na hivyo akahamia nchini Uswisi pamoja na mkewe. Msanii huyo katika tasnia ya filamu alifariki dunia mwaka 1977.
Miaka 68 iliyopita katika siku kama ya leo waisrael waliokuwa na silaha walishambulia kambi ya zamani wa askari wa Uingereza huko Palestina na kuua Wapalestina 90 na kujeruhi wengine wengi. Kwa upande mmoja, maafa hayo yalitokea wakati askari wa Uingereza walipokuwa wakiondoka katika kambi hiyo na kurejea nchini kwao, na kwa upande wa pili, waisraeli walikuwa wameshadidisha mauaji hayo ya Wapalestina wasio na hatia kwa lengo la kuasisi dola haramu la Israel.

KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA