Leo ni kivumbi New York katika Kampeni | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Tuesday, April 19, 2016

Leo ni kivumbi New York katika Kampeni

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
ImageGetty Images
ImageWagombea wa Democrat Hillary Clinton na Bernie Sanders.
Wagombea waliobaki kwenye kinyanganyiro cha kuwania urais nchini Marekani, wanang'ang'ania kura muhimu zaidi za mchujo hii leo katika jimbo la New york. Likiwa moja ya majimbo makubwa nchini Marekania lina ushawishi mkubwa kwa wagombea wote.
Kwa wagombea wa chama cha Democtrats Bernie Sanders amelelewa mjini New York naye Hillary Clinton amekuwa seneta katika jimbo hilo.
Kwa upande wa Republican mgombea mkuu Donald Trump ni mwenyeji wa jimbo hilo.
Ananuia kupata ushindi dhidi ya mshindani wake mkuu Ted Cruz, Lakini amekosoa mbinu ya kumchagua mgombea wa chama.
ImageReuters
ImageWagombea wa Republican Donald Trump na Ted Cruz
Wagombea hao wote wamekuwa kwenye kampeni ya kuwarai wapiga kura. Clinton aliwaambia wapiga kura kuwa hatachukulia chochote kwa msaha huku kwa upande wa Republican Trump akisisitiza mapenzi yake kwa jimbo la New York.
Mshindani wake mkuu Ted Cruz hatarajiwi kufanya vyema baada ya kukosoa sera za Trump mapema kwenye kampeni.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA