MKURUGENZI WA HALMASHAURI WA MJI KAHAMA APEWA SIKU TISINI NA WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AWE AMENUNUA MASHINE YA MIONZI X RAY. | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Saturday, April 16, 2016

MKURUGENZI WA HALMASHAURI WA MJI KAHAMA APEWA SIKU TISINI NA WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU AWE AMENUNUA MASHINE YA MIONZI X RAY.

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Mkurugenzi wa halmashauri wa mji kahama amepewa siku tisini awe amenunua mashine ya mionzi (x ray)kwa ajili ya hospitali ya mji kahama.Agizo hilo amepewa jana na Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy mwalimu wakati alipotembelea hospitali hiyo pamoja na kuongea na watumishi wa kada ya afya wa wmji huo.

Waziri Ummy alisema ametoa agizo hili ili kuweza kurahisisha usumbufu wanaupata wananchi wa wilaya hiyo kwa kwenda kupata huduma nje ya hospitali ambapo wakati mwingine vipimo hivyo vinakuwa havisomeki vizuri kwa kukosa viwango vinavyostahili za mashine hizo.

Hata hivyo waziri ummy alisema upatikanaji wa mashine hizo itapunguza malalamiko mengi toka kwa wananchi kwa ukosefu wa kifaa tiba hicho ili kwani hospitali hiyo hivi sasa inahudumia wananchi zaidi ya milioni moja hususan toka wilaya zote za wilaya hii.

Aidha, alizitaka halmashauri zote mjini kuweza kuwekeza kwenye huduma za vifaa tiba ambavyo inarahisisha kugundua matatizo yanayowakabili wananchi wanaofika kwenye kupata huduma na hivyo kuwapatia matibabu stahili wagonjwa wanaofika kupata matibabu kwenye vituo vya kutolea huduma nchini.

?siku hizi lazima muwekeze kwenye kununua vifaa tiba ili kuweza kupata kutoa huduma nzuri ,pesa mnakusanya na kahama ni halmashauri tajiri,mkurugenzi nakupa siku tisini uwe umenunua mashine hiyo.

Naye mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Vita kawawa amemuahidi waziri huyo kwamba amepokea maagizo yote aliyoyatoa na atayafuatilia ili kuweza kutatua malalamiko ya wananchi na yale ya watumishi wa kada ya afya.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akiongea na baadhi ya wakazi wa kahama waliofika hospitalini hapo kuangalia wagonjwa wao.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh.Vita Kawawa(Katikati) akionesha kwa vitendo bango hilo linapotakiwa kuwekwa,kushoto ni Mh.Ummy Mwalimu na kulia ni mkurugenzi wa halmashauri ya mji kahama Anderson Msumba.

Mfamasia Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Luciano Lodrick akimpatia maelezo waziri ,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto jinsi ya utengenezaji wa maji tiba.
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA