Watatu wakamatwa kwa kusafirisha wahamiaji haramu | MAUJANJA 24 NEWZ

HABARI ZA KITAIFA,KIMATAIFA,KUMBUKUMBU ZA KIHISTORIA,MICHEZO NA BURUDANI,NA MENGINE MENGI

Breaking News
Loading...

Saturday, April 16, 2016

Watatu wakamatwa kwa kusafirisha wahamiaji haramu

Kama Bado Hujajiunga Nami, Unaweza Kujiunga Kwa Kubonyeza Like Hapa Chini Nikutumie Habari Moja Kwa Moja
Tanga. Watanzania watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Tanga wakituhumiwa kuendesha biashara ya kuwasafirisha kwa kutumia gari aina ya hiace wahamiaji haramu 10 kutoka nchini Ethiopia.

Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga ,Leonard Paulo amesema leo kuwa watanzania hao pamoja nawahabeshi wamekamatwa jana saa 2.30 usiku katika eneo la Misajini barabara kuu ya Hedaru- Mombo.

Amesema kuwa wahamiaji hao walimatwa wakati askari wakiwa doria waliokuwa wakisafirishwa kwenye gari aina Toyota Hiace iliyokuwa ikiendeshwa na Ally Juma (24) mkazi wa Dar es Salaam wakiingia mkoani hapa.

Amewataja watanzania wengine wawili ambao wamekamatwa wakituhumiwa kuwakisafirisha wahamiaji haramu hao kuwa ni Joseph John (42) mkazi wa Mkoa wa Dar es Salaam na Iddi Juma(38) mkazi wa mkoani Iringa.

Ametaja majina ya Wahabeshi waliokuwa wakisafirishwa kuwa ni
Tarfa Wolder (21),Aramei Yonas (21),Gazae Edson(20),Yohanes Abakar (27),Anemo Tamire (16),Indira Yaiso(18),Wasifimu Paresa (15),Dedacho Gadam (20),Tamelata Abala (17) na Mlatu Shugute (32).
KUPATA HABARI NA MATUKIO YA KILA SIKU, BONYEZA Like HAPA CHINI
Asante! TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

google+

linkedin

Maujanja Yote Tz Blog
  • Karibu katika Mtandao Huu unaotoa Habari Za Uhakika Kutoka Ndani Na Nje Na Tanzania. Kama una Tangazo,Habari,Picha,Ushauri n.k Wasiliana nasi kwa simu namba 0755-207374. Soma Zaidi

    0 comments:

     

    IDADI YA WASOMAJI

    TAFUTA HABARI HAPA